Header Ads

Wanasayansi 200 Kuonesha Kazi Zao Jijini Dar

                       

Maonesho ya elimu ya Sayansi kwa wanafunzi wa Sekondari maarufu kwa jina la 'Young Scientist' yanataraaji kuanza agosti 8 hadi 9 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Young Scientist Tanzania(YST), Dr Gozibert Kamugisha amesema onesho hili la aina yake na litaonyesha kazi za kisayansi na ugunduzi kutoka kwa wanafunzi wa Sekondari 200 na walimu 100 kutoka mikoa yote Tanzania.

“kwa siku mbili za onesho wanasayansi Chipukizi wataonesha kazi zao katika Nyanja mbalimbali za Sayansi kama vile kemia, fizikia, hesabu, Bailojia, ekolojia, Sayansi ya Jamii na Teknonojia. hivyo kazi nyigi zitakazooneshwa zimejikita katika kutoa njia za kukabiliana na matatizo ya afya, Kilimo na usalama wa matatizo ya kijamii zaidi”Amesema Kamugisha.

Amesema Onesho hilo limewezeshwa na udhamini endelevu wa BG Tanzaniaa ambayo ni kampuni tanzu ya Royal Dutch ShellPlc na wadhamini wengine. Ametaja kuwa Wanasayansi Chipukizi watakaonesha kazi nzuri watazawadiwa pesa Taslimu ,Vikombe ,Medali na Vifaa vya Maabara.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shell Afrikaa ya Mashariki na Bg Tanzaniaa, Marc den Hartog amesema kuwa wao kama Shell wanaona fahari kubwa kuwa mdhamini wa mashindno hayo kwa kwa kufanya hivyo ndivyo wataweza kupata wanasayansi wa baadae ambao wataweza kusaidia katika uchumi wa Viwanda na sekta ya gesi na mafuta .

No comments