Header Ads

Msuva: Nataabika hakuna ugali Morocco

 Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ambaye anayechezea klabu ya Difaa El Jadida ya nchi ya Morocco amefunguka kuwa anapata shida ya chakula kutokana na kukosekana kwa ugali nchini humo.

Msuva amebainisha hayo baada ya kufanyiwa mahojiano maalum na mwandishi wa habari ambapo ameelezea vitu vingi anavyoviona vya tofauti tokea afike nchini humo ambapo kwa sasa ndipo anapochezea soka la kulipwa.
"Hali ya hewa ya huku Morocco haina utofauti na ya Dar es Salaam nilipokuwa nikichezea klabu yangu ya Yanga ila kwa upande wa vyakula huku ugali hakuna kabisa japokuwa kuna wali ila upikwaji siyo kama wa huko nyumbani Tanzania", amesema Msuva.

Kwa upande mwingine, Msuva siku ya leo amekabidhiwa jezi rasmi na klabu yake mpya ya Difaa El Jadida yenye namba 27 mgongoni sawa na ile aliyokuwa akiiva katika klabu ya Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans, ambapo atanza kuitumia pindi ligi kuu nchini humo itakapoanza.

No comments