Header Ads

ACT Wazalendo waandaa mkutano wa ujenzi wa taifa



Chama cha ACT-Wazalendo kimeandaa mkutano utakaohusu ujenzi wa taifa huru la kidemokrasia na maendeleo endelevu.

Akizungumza leo Jumapili,Naibu Katibu wa chama hicho upande wa Tanzania Bara,Msafiri Mtemelwa amesema mkutano huo utafanyika Agosti 26 jijini Mwanza.

Amesema Katiba ya chama hicho inaeleza wazi kuwa kutakuwa mkutano wa kidemokrasia utakaokuwa jukwaa la masuala ya kisiasa,uchumi na utamaduni.

Amesema viongozi mbalimbali wa vyama kama Die Linke cha Ujerumani na Labour cha Uingereza watakuwepo kwenye mkutano huo na watatoa mada kuhusu uzoefu wa vyama vyao."Tunatumia fursa hii kuwakaribisha watanzania wote kushiriki kwenye mkutano huu wa kihistoria.

No comments