Wachezaji Yanga na Simba kupimwa kama Wanatumia Madawa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema wachezaji wote watakaochezwa mechi ya Ngao ya Jamii ya watani Yanga na Simba, watachukuliwa vipimo.
Lengo la TFF ni kuwapima wachezaji wote ili kuangalia kama kuna wale wanaotumia madawa haramu ya kuongeza nguvu.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema lengo lao ni kuufanya mchezo kuwa fair kiuchezaji na anayeshinda, ashinde kwa haki.
“Hata hivyo hatujasema kwamba kuna timu fulani wachezaji wake wanatumia dawa, badala yake hii ni katika kujiridhisha tu,” alisema.
Tayari TFF imetangaza kuwa mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, itaanza saa 11 jioni ikiwa imesogezwa mbele kwa saa moja.
Simba waliweka kambi Unguja na Yanga wako Pemba na sasa kinachosubiriwa ni “Show Time”.
Post a Comment