Mke wa Roma: Naahidi kukupa style zote
Mke wa msanii wa Roma, Nancy ametoa ahadi yenye utata kidogo kwa mumewe mara baada ya video yake ‘Zimbabwe’ kufikisha views milioni moja.
Siku ya jana August 20, 2017 video ya Roma ilifikisha idadi hiyo ya views katika mtandao wa YouTube tangu ilipoweka katika mtandao huo August 10 mwaka huu. Kitendo hicho kilimchanganya Baby Mama huyo na kukimbilia katika mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe mfupi;
Finally You Made It #1Milion_Views Ndani ya Week 1 Na siku 3!!!😘😘 Walahi Mume wangu @roma_zimbabwe#LEO_NITAKUPA_STYLE_ZOTE Kwa Furaha Niliyonayo!!! Hongera Mno!! Much Congrat kwa shemela @nicklassm Nakuona Mbali Saaana!!
Video hiyo hadi sasa ina views 1,040,849, hata hivyo imetoa katika trending baada ya kukaa katika number one trending kwa wiki moja. Lakini video mpya ya Rostam (Roma & Stamina) ‘Hivi Ama Vile’ ameanza kufanya vizuri ambapo kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika trending.
Post a Comment