Roma Mkatoliki atoa siri ya Zimbabwe
Rapa Roma amedai sababu za kusema anakwenda Zimbabwe ni kutokana na ukweli kwamba nchi hiyo ni moja kati ya nchi ambazo ziliguswa na matatizo aliyopata ikiwepo kutekwa na kuteswa kwa siku tatu mfululizo.
Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Roma amesema ingawa tayari idea ya wimbo huo ilikuwepo lakini alitamani kuonyesha mama wa Afrika kwani Zimbabwe ni kati ya nchi ambazo Tanzania ilisaidia kutafuta uhuru wake.
"Ningeweza kwenda Zimbabwe au nchi nyingine yoyote Afrika lakini nilitaka kuonyesha Mama wa Afrika, ukizingatia Rais Mandela na Nyerere tayari wameshaondoka lakini Mugabe yupo hai.
Nilipopata matatizo watu wa nchi mbalimbali walipaza sauti zao ili tuliokuwa tumetekwa tupate kurudi tukiwa hai, kwa hiyo nikaona bora iwe Zimbabwe ingawa tayari idea ya wimbo huu ilikuwepo muda mrefu kidogo" Roma.
Pamoja na hayo Roma amefunguka na kusema wanaodhani kuwa Zimbabwe ni kubwa kuliko ngoma zake zote wanakosea kwani wakati alipoingia kwenye game wimbo wake wa kwanza uliposikika redioni alipokea simu nyingi za nje ya nchi kiasi cha kujihisi anaweza akaimba matatizo ya wananchi wa Afrika na yakapatiwa ufumbuzi.
Hata hivyo Roma ameweka wazi kuwa bado anasafari ya Zimbabwe lakini hawezi kusema anakwenda kufanya nini kwani ni mambo binafsi zaidi ingawa pia akimaliza 'media tour' ataondoka tena
Post a Comment