Kenya: Marafiki wa NASA wafukuzwa
Kiongozi wa Nasa na mgombea nafasi ya Seneta Kaunti ya Siaya amesema marafiki zao kutoka nje ya nchi wamefukuzwa nchini.
Kiongozi huyo James Orengo amesema marafiki zao wanne wawili kutoka Ghana na wengine wawili mmoja anatoka Marekani mwingine Canada walirudishwa katika nchi zao juzi usiku.
Orengo alisema waghana wao walirudishwa wakiwa bado uwanja wa ndege na wengine wawili mcanada na mmarekani wao walikamatwa kwenye kituo cha Nasa cha kukusanya matokeo kilichopo Westlands na kurudishwa walikotoka.
Alisema wametoa taarifa kwa ofisi za ubalozi wanakotoka raia hao.
Alipoulizwa sababu za kuleta marafiki wa kigeni kwenye shughuli za uchaguzi, alijibu kuwa hiyo ni kama Jubilee walivyomwalika rafiki yao Edward Lowassa kwenye mkutano wao wa kampeni.
Post a Comment