Manara amvaa Kamusoko
Afisa habari wa mabingwa wa kombe la Ngao ya Jamii Simba Sc, Haji Manara amefunguka na kudai kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe wa Yanga Thabani Michael Kamusoko hana hadhi ya kucheza mpira katika vilabu vya Tanzania bali alipaswa kuchezea timu za Ulaya
Manara amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Instagram baada ya kuona jitihada na umahili mzuri wa Kamusoko wa kucheza mpira pindi awapo uwanjani.
"Huwa sifichi mahaba yangu kwa mchezaji anayenivutia uwanjani hata kama anachezea klabu nisiyoishabikia. Scara Kamusoko hapewi heshima anayostahili nchi hii. 'Level' yake ni kucheza Ulaya", aliandika Manara.
Thabani Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji wa klabu ya Yanga waliyoweza kuipigania timu yao katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Ligi Kuuu Tanzania Bara jana dhidi ya Lipuli FC na hatimaye kutoka sare ya mabao 1-1 mchezo ulipigwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment