Mwanamuziki Ali Kiba Awashika masikio
ALI KIBA
STAA anayekimbiza na Wimbo wa Seduce Me, Ali Kiba Saleh ‘King Kiba’ ametupa jiwe gizani kwa kusema, hana tabia ya kutelekeza watoto kama mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva anavyofanya. Kiba ambaye wiki iliyopita alikuwa nchini Marekani kikazi, alifungukahayo alipokuwa akipiga stori mbili tatu na Ijumaa Wikienda kuhusiana na maisha yake ya kimuziki.
Kiba alisema kuwa, katika maisha yake, japo Mungu hajamjalia kufunga ndoa, lakini kwa watoto watatu ambao tayari amewapata, anahakikisha anawalea vizuri na wanapata mahitaji muhimu na kamwe hawezi kutelekeza damu yake. “Mimi kiukweli katika eneo hilo ninamshukuru Mungu. Wanangu ninawalea vizuri na ninahakikisha wanapata kila kitu kinachostahili katika suala zima la malezi.
“Uzuri ni kwamba mimi ni Muislam, ninawalea pia kwa misingi ya dini yangu kwa kuhakikisha wanasoma madrasa na wanaishi katika misingi ya kumjua Mungu,” alisema Kiba. Baada ya kusema hayo, Kiba alizidi kupigilia msumari maneno yake kwa kumwambia mmoja wa wasanii ambaye anatajwa katika ishu za kutelekeza watoto awe makini kwani kuiachia damu yake ipotee bure ni dhambi. “Mimi sitelekezi watoto kama yeye bwana, abadilike pia ikibidi maana siyo ishu kutelekeza damu yako bwana,” alisema Kiba.
Alipobanwa Kiba amtaje msanii huyo alisema haina sababu ya kumtaja kwa sababu mashabiki wake wenyewe ni waelewa, wataelewa tu anamaanisha nani. “Hakuna sababu bwana ya kumtaja, kwani hata wewe si ushajua? Tumstahi kwa sasa,” alisema Kiba. Japo Kiba hakumtaja, Ijumaa Wikienda lilifanya upembuzi wake na kubaini kwamba, yupo msanii mmoja wa Bongo Fleva ambaye ana sifa hiyo ya kukataa watoto wake (tukikamilisha ushahidi tutamuanika).
Post a Comment