Header Ads

AWAMU YA TANO YAONESHA UTOFAUTI, TUSUBIRI UTEKELEZAJI.



Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai ameonyesha kushangazwa na bajeti iliyowasilishwa bungeni leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.

“Kwa kweli hii haijawahi kutokea, ni kwa miaka mingi hatujawahi kuona bajeti nzuri kama hii.” amesema Ndugai.

Ndugai ameyasema hayo leo (Alhamisi) mara baada ya Waziri Mpango kuhitimisha kuwasilisha bajeti kuu ya mwaka 2017/18 huku asilimia kubwa ya wabunge wakimpigia makofi Waziri huyo.

Ndugai ameisifia bajeti hiyo akisema kwa miaka mingi ya uwasilishwaji wa bajeti za Serikali bungeni haijawahi kutokea wabunge wakaipokea vizuri kiasi hicho

No comments