AIPALILIA NAFASI YAKE
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amemmwagia sifa Rais John Magufuli kuwa ni kiongozi mwenye uthubutu wa kufanya mambo mapya bila woga.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi) wakati akihitimisha uwasilishaji wa bajeti kuu ya mwaka 2017/18 na kueleza kuwa Rais Magufuli ana uzalendo, anaipenda nchi yake kwa moyo na anajitoa.
Pia, Dk Mpango amesema miongoni mwa mambo mazuri aliyoyafanya Rais Magufuli yalikuwa machungu kwa baadhi ya watu.
“Tujielekeze kutekeleza dira ya maendeleo, tulinde rasilimali na kulinda umoja na amani yetu kama mboni ya jicho kama anavyofanya Rais wetu,” amesema.
Ameyataja mambo hayo kuwa ni kutengua uteuzi wa baadhi ya viongozi, kuweka nidhamu katika sekta za Serikali na kuzuia matumizi yasiyo ya lazima katika taasisi za fedha.
Pia, amemsifu JPM kwa kuanzisha mchakato wa kuhamia Dodoma, ujenzi wa barabara ikiwamo barabara za juu, ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga na kuchunguza sakata la mchanga wa madini.
Post a Comment