Serikali imepiga marufuku shule hizi
Mh Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo baada ya kukagua shule ya sekondari Mwandiga ambayo inatarajiwa kupokea kwa mara ya kwanza wanafunzi wa sayansi 143 wa kidato cha tano,ambapo ameagiza idara ya ukaguzi kufanya ukaguzi na kutoa kibali kabla shule kupokea wanafunzi.
Mapema Mkuu wa shule ya sekondari Mwandiga Albert Mutwe alieleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa huduma ya maji,bwalo, usafiri, nyumba za walimu na maktaba huku mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga akiahidi kukamilisha miundombinu ya shule hiyo ili wanafunzi waweze kuanza kidato cha tano.
Post a Comment