Header Ads

Wito wa Kenyatta kwa Wakenya

                                          

Aliyekuwa Rais wa nchi ya Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa wapiga kura nchini humo siku ya leo kuondoka mapema kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kumaliza ili kuepukana na purukushani zitakazoweza kujitokeza katika maeneo ya kupiga kura.

Kenyatta amesema hayo katika hotuba yake ya mwisho kwa taifa hilo ambapo alisema wananchi wanapaswa kupiga kura kwa amani na utulivu bila ya kupatwa na shida ya aina yoyote ili waweze kujichagulia kiongozi wanaye muhitaji.

"Ombi langu kwa wakenya wote, tujaribu kupiga kura kwa amani na mkumbuke kurudi majumbani kwetu mapema", alisema Kenyatta.

Hata hivyo, uchaguzi wa Kenya umewagharimu walipakodi wa nchi hiyo takribani shilingi bilioni 49 ambapo umeelezwa kuwa ghali zaidi ikilinganishwa na uchaguzi katika mataifa jirani.

Kwa upande mwingine, matokeo ya awali ya uchaguzi huo hayatarajiwi kutolewa kabla ya siku ya kesho (Jumatano), kwa mujibu wa katiba, Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kwa kuwa Tume ya uchaguzi ina hadi siku saba kumtangaza mshindi.

No comments