Polisi amnunulia mwizi nguo alizoshikwa akiiba dukani
Alisema kuwa wakati alifika eneo hilo aligundua kuwa mtu huyo alikuwa akiiba nguo ili avae akienda kufanyiwa mahojiano ya kutafuta ajira
Mwizi wa duka huko Toronto ambaye alishikwa akiiba nguo ili aweze kuivaa kwa usaili alipata fusra asiyoitarajia kutoka kwa polisi ambaye aliitwa kuja kumkamata.
Niran Jeyanesan aliambia kituo cha habari cha CP24 kuwa mfanyakazi wa duka la Walmart, aliripoti kuwa mtu huyo wa umri wa miaka 18 alijaribu kuiba shati, tai na soksi.
Alisema kuwa wakati alifika eneo hilo aligundua kuwa mtu huyo alikuwa akiiba nguo ili avae akienda kufanyiwa mahojiano ya kutafuta ajira.
"Kijana huyu amekuwa akikumbwa na wakati mgumu maishani na anajaribu kutatua hilo kwa kuitafutia familia yake riziki kwa kujaribu kupata kazi," bwana Jeyanesan alisema.
Akiongea na BBC mkuu wa Jeyanean, Paul Bois alipongeza kitendo hicho chake.
Post a Comment