Header Ads

Neymar afunguka mazito kuhusu Messi

                            

Hakuna marefu yasiyo na ncha, MSN imemeguka baada ya N kuondoka,Messi, Suarez na Neymar ni utatu ambao hakuna beki yoyote duniani ambaye angependa kukutana nao, huu ni muunganiko hatari zaidi kuwahi kuushuhudia katika ulimwengu wa soka.

Lakini sasa Suarez na Messi wamebaki wapweke baada ya muuaji mwenzao kutua PSG kwa mkataba wa miaka 5, Messi, Suarez na Neymar walikuwa kama ndugu chemistry iliyokuwa kati ya wanyama hawa watatu ulikuwa inatishia sana usalama wa wapinzani.

Baada ya Neymar kuondoka Barcelona alianza Messi kwa kuandika majonzi yake na jinsi anavyojisikia vibaya kumpoteza Neymar ambaye alikuwa kama rafiki kwake,Neymar naye amemuandikia ujumbe Messi, Suarez na Barca jinsi anavyojisikia kuondoka, ujumbe ambao umewaumiza zaidi mashabiki wa Barcelona.

“Maisha ya soka yamejawa na changamoto nyingi sana ikiwemo matokeo na nyingine za nje ya uwanja lakini Barcelona kumekuwa na changamoto nyingi sana, nakumbuka nilifika nikiwa kijana mdogo tu mwenye miaka 21” alianza kwa kuandika Neymar.

“Siwezi sahau siku yangu ya kwanza kufika Nou Camp na kushare chumba na watu niliotamani kuwa kama wao akiwemo Iniesta,Puyol,Valdes bila kumsahau Messi, hakika ilikuwa faraja kwangu kucheza Barcelona ni zaidi ya timu”

“Najisikia faraja sana kuwahi kucheza na mchezaji bora kuwahi kumuona na sidhani kama nitakuja kuona kama Lioneil Messi na alikuwa rafiki yangu nje na ndani ya uwanja, yeye na Suarez walinifanya nishinde kila kitu ambacho mchezaji anataka kushinda”

“Lakini hili ni soka na kama mwanasoka nahitaji changamoto mpya na kwa mara ya pili ninapingana na baba yangu na kufanya ninachoona ni sahihi na naamini utanisuport,Barcelona iko moyoni mwangu lakini nahitaji changamoto mpya PSG”

Neymar alimalizia kwa kusema ni uamuzi mgumu alioufanya lakini kwa umri wake wa miaka 25 anaona ni jambo sahihi na pia amefuta minong’ono ya kwamba baba yake ndio amelazimisha usajili huo ufanyike lakini kumbe baba yake hakutaka Neymar acheze PSG.

No comments