Zawadi waliyoahidiwa Juventus wakishinda Champions League leo
Usiku wa June 3 2017 mchezo wa fainali ya UEFA Champions League msimu wa 2016/2017 ndio utachezwa katika uwanja wa Millenium jijini Cardiff nchini Wales kwa kuzikutanisha timu za Real Madrid dhidi ya Juventus.
Huu ni mchezo ambao unatajwa kuwa na mvuto zaidi kwa siku ya leo kutokana na historia ya michuano hiyo ambayo ni mikubwa barani Ulaya, kuelekea game hiyo beki wa Juventus Dani Alves ameweka wazi zawadi waliyoahidiwa na Rais wa club yao.
Juventus kama watafanikiwa kutwaa Ubingwa wa UEFA Champions League msimu wa 2016/2017 dhidi ya Real Madrid wameahidiwa na Rais wa Club yao kuwa wachezaji watapewa Ferrari wakifanikiwa kushinda taji hilo.
Post a Comment