Anna Mghwira ateuliwa kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro
Bibi Anna Mghwira anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Saidi Meck Sadiki aliyekuwa mkuu wa mkoa huo.
Bi Mghwira alikuwa mgombea pekee wa kike wakati wa kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015.
Amekuwa mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, chama kichanga zaidi Tanzania kilichoundwa 2014.
Mghwira, 56, anatoka mkoa wa Singida. Babake alikuwa diwani na kiongozi chama cha Tanu na baadaye CCM.
Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor alikuwa mkuu wa oparesheni na mafunzo wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania.
Halikadhalika Rais magufuli amemteua DIGP Abdulrahman Omar Juma Kaniki kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo DIGP Abdulrahman Omar Juma alikuwa mkuu wa jeshi la polisi.
Post a Comment