Header Ads

Wanajeshi 60 wauawa



Wanajeshi 61 wahofiwa kuuwa na Al-Shabaab Puntland, Somalia.

Kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Al -Shabab, linasema kuwa limewauwa askari 61 katika kambi moja ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Bosaso nchini Somalia.

Idara ya BBC Monitoring, inanukuu vyanzo viwili vya habari kutoka kwa makundi yanayounga mkono Al-Shabab.

Kambi hiyo ya kijeshi ipo katika eneo la jimbo lililojitangazia uhuru wake la Puntland.

Mwaandishi mmoja pia wa VOA ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa tweeter kuhusiana na shambulio hilo.

Utawala huko Puntland umethibitisha kutokea kwa shambulio hilo lakini unapinga idadi ya waliouwawa.

Duru zasema kuwa shambulio hilo la mapema Alhamisi asubuhi, lilitokea karibu na milima ya Galgala, ambao hapo awali ilikuwa ngome ya wapiganaji wa al-Shabab katika jimbo hilo la Puntland.

Kufikia sasa, bado hakujatolewa idadi rasmi ya waliouwawa, lakini waziri wa ulinzi wa Abdiaziz Hirsi amekanusha madai ya al-Shabab.

Anasema kuwa mamlaka inaendelea kuchunguza swala hilo na itatoa taarifa ya kina muda mfupi baadaye.

Mwaandishi wa BBC wa idhaa ya Kisomali Jiijini Nairobi Mohammud Ali ambaye anafuatilia taarifa hiyo, amesema kuwa jimbo la Puntland limekuwa likikumbwa na mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa al-Shabab, lakini hili la sasa limetajwa kuwa baya zaidi katika siku za hivi karibuni.

No comments