Header Ads

DOGO JANJA ATEMA CHECHE


Rapa kutoka 'Tip Top Connection' anayewakilisha A City, Dogo Janja amefunguka na kusema kwamba katika matumizi ya mitandao ya kijamii anaogopa sana watu wanapo hariri (edit) picha kuwa kuongeza au kupunguza kitu kwenye sura ya mtu.

Janjaro amefunguka na kuweka wazi kwa kusema kwamba suala la matusi mitandaoni halimuongopeshi kutokana na mazingira aliyokulia lakini linapokuja suala la kuongezeana au kupunguziana vitu kupitia picha zilizopo mitandaoni huwa zinamuumiza na kumuogopesha.

"Suala la kutukanwa nimezoea sana, kwani sijaanza kutukanwa jana au leo kwa sababu mazingira niliyotokea mimi baba anaweza akamtukana mama mbele ya watoto. Ila linapokuja suala la mtu kukuwekea 'shape' kwenye mwili wako au kukupaka make up na kukugeuza kama mwanamke huwa naogopa sana pia zinaniumiza" alifunguka Dogo Janja.

Kwa sasa msanii huyo ana-'hit' na ngoma inayokwenda kwa jina la 'ukivaaje unapendeza' iliyotengenezwa na prodyuza Daxo Chali Kutoka AM records

No comments