Header Ads

Umoja wa Mataifa yaiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa kauli moja kuongeza watu 15 na mashirika manne yanayohusishwa na mpango wa nyuklia na makombora wa Korea Kaskazini kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
 Hata hivyo, upinzani wa China ulizuia vikwazo vipya vikali ambavyo vilikuwa vikishinikizwa na Marekani. 
Wakati azimio hilo litawawekea marufuku ya kusafiri ulimwenguni na kuzuia mali za baadhi ya Wakorea Kaskazini, halitalenga usambazaji muhimu wa mafuta au kujumuisha vikwazo vingine vikali, hatua ambayo utawala wa Marekani ulitaka ichukuliwe dhidi ya Korea Kaskazini. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.
 Nikki Haley aliziomba nchi zote kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Korea Kaskazini. Kwa upande wake, Balozi wa China Liu Jieyi alisisitiza kuwa azimio hilo lilielezea umuhimu wa kudumisha amani na usalama katika Rasi ya Korea na kaskazini mashariki mwa Asia na akaelezea nia ya baraza la usalama ya kutafuta suluhisho la amani la kidiplomasia na kisiasa, na umuhimu wa kupunguza mivutano

No comments