Header Ads

Dawa ya kutibu saratani ya ovari yafanyiwa majaribio

Marianne Heath
Image captionMarianne Heath alipata matibabu kwa muda wa miezi sita, na dawa hiyo ikapunguza uvimbe wote kati mwili wake
Watafiti nchini Uingereza wanasema majaribio ya awali ya dawa ya kukabiliana na saratani ya ovari yameonyesha matumaini makubwa.
Wanawake 15 walihusika katika majaribio hayo na baada ya miezi mitano, uvimbe kwenye ovari za wanawake saba ulipungua kwa kiwango kikubwa baada ya kutumia dawa hiyo.
Dawa hiyo inashambulia seli mbaya pekee.
Saratani ya ovari huwa si rahisi kutibu, na japo wanasayansi wanasema dawa hiyo sio tiba halisi, itasaidia pakubwa kurefusha maisha ya wagonjwa
Marianne Heath, mwenye umri wa miaka 68 ambaye alitibiwa kwa kutumia dawa hiyo alisema, "sikuwa na njia nyingine, kwa hivyo nilihisi kuwa ndilo chaguo langu tu.
Marianne alipata matibabu kwa muda wa miezi sita, na dawa hiyo ikapunguza uvimbe wote kati mwili wake na kuondoa maumivu yote aliyokuwa akihisi.
Ovarian cancerHaki miliki ya pichaSPL
Image captionSaratani ya ovari inaweza kuwa ngumu kutibu

No comments