Ronaldo akaribia kuchukua Ballon d' Or
Mshambuliaji wa Real Madrid, Christiano Ronaldo amethibitisha ubora wake, baada ya kufunga mabao mawili kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi.
Ushindi huo wa mabao 4-1 umemuibua Rais wa Real Madrid, Florentino Perez akisema, Ronaldo ndiye anastahili kupata Tuzo ya Ballon d’Or msimu huu.
Ronaldo amefanikisha Madrid kutimiza ndoto yake ya kutwaa mataji mawili makubwa msimu huu.
Madrid ilicheza mbele ya Juvenus pungufu baada ya mchezaji wake kulimwa kadi nyekundu, huku vijana wa Zinedine Zidane wakipata uchochoro zaidi wa kuziona nyavu.
Kutokana na ubingwa huo, Real Madrid imefikisha mataji mawili baada ya kunyakua ubingwa wa La Liga msimu huu.
Kwa maana hiyo, Perez alisema hakuna sababu ya kumzuia Ronaldo kutwaa tuzo ya Ballon d’Or.
Post a Comment