Agizo La Majaliwa Latekelezwa...
HALMASHAURI ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani itaanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kuhusu kuhakiki mipaka inayotenganisha vijiji na Hifadhi ya Saadani mara baada ya mvua kumalizika.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Zikatimu katika Baraza la Madiwani akitolea ufafanuzi iliyokuwa inazungumzia migogoro ya mpaka kati ya wananchi wa vijiji husika na Hifadhi ambapo alisema mara baada ya mvua hizo kwisha kazi hiyo itaanza mara moja.
Baraza hilo likihudhuliwa na Mhifadhi Mwandamizi wa SANAPA Lumi Ole Naikasi, madiwani hao walitaka kufahamu kutoka kwa Mhifadhi huyo kwamba ni lini mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi na wananchi hao utamalizika, wengine wakiulizia hatima ya malipo kwa wananchi ambao wametoa maeneo yao kwa hifadhi hiyo.
Rehema Mno alizungumzia suala linalohusiana na tozo ya sh. 5,000 kwa wananchi wanaokwenda kwenye vijiji hivyo kuangalia familia zao ambao wanapofika katika mlango wa kuingia ndani ya hifadhi wanatizwa fedha jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi hao.
Sijali Mpwimbwi alitaka kujua hatma ya migogoro ya mipaka kati ya wananchi na Hifadhi pia malipo ya fidia kwa waliotakiwa kuondoka kwenye maeneo yao, huku Hussein Hading'oka akisema ingawa Hifadhi imewekwa kwa makusudi maalumu kwa mujibu wa sheria na Taratibu, huku ikiwakuta wananchi, sasa imekuwa kero kwao.
"Saadani haina tofauti na Hifadhi nyingine, nichukulie mfano ya Mikumi ina urefu wa zaidi ya kilomita 50 kutoka kona mpaka kona lakini watu wanapita muda wote hakuna kuzuiwa, iweje Saadani wananchi wetu wazuiwe baada ya saa 12 za jioni?," alihoji Hading'oka.
Juma Mpwimbwi alisema kuwa Halmashauri inamiliki kilometa 45 za barabara wakati TANAPA ina kilometa si zaidi ya 12, lakini wanatoza uahuru kwa kila gari zaidi ya sh. Laki moja, barabara zinapoharibika hawafanyi mateengenezo hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wanaosafiri kwa magari, huku akigusia kuzuiliwa kwa gari la kubeba wagonjwa kuoita enwo hilo.
"Cha kusikitisha zaidi hata panapotokea mgonjwa wakipiga simu kwangu ili gari ya wagonjwa iende, ikifika mlangoni wanaizuia wakieleza muda wa kupita eneo hilo unekwisha, wale ndugu zetu wataishije? Alihoji Mpwimbwi.
Akizungumzia malalamiko hayo, Mhifadhi Lumi alisema kuwa suala la ushuru wa kuingia ndani ya eneo la Hifadhi upo kisheria hivyo wao hawawezi kutengua, kuhuau mipaka wao wameikuta, wakati upande wa fidia kwa wananchi kufuatia maeneo yao kuchukuliwa, wapo tayari kuwalipa wanachosubiri ni taratibu.
Akihitimisha mjadala huo, Zikatimu alisema kwamba kuhusu mipaka kuna maelekezo yametolewa na Waziri Mkuu Majaliwa na kwamba mara baada ya mvua za masika kaI hiyo itafanyika.
Post a Comment