Biashara ya Pombe yashuka kote Duniani
Idadi ya watu wanaojivinjari kwa mvinyo imepungua, kulingana na ripoti ya shirika mpya linalofuatilia unywaji wa pombe duniani.
Uuzaji wa pombe uliendelea kudidimia mwaka jana huku pombe ya Cider iliyoanza kupata maarufu sasa hainunuliwi kama hapo mwanzoni.
Soko la kimataifa la pombe lilipingua kwa asilimia 1.3 mwaka wa 2016, hali iliyosababishwa na kushuka kwa ununuzi wa pombe kwa asilimia 1.8.
Uuzaji wa pombe ya Cider ulishuka kwa asilimia 1.5 baada ya miaka kadhaa ya kufanya vizuri.
Kulingana Shirika la fedha duniani, kukua kwa uchumi wa nchi huwa inaachangia kuongezeka kwa unywaji wa pombe.
Uuzaji wa pombe nchini China ulishuka kwa asilimia 4.2, huku nchini Brazil na Urusi ukishuka kwa asilimia 5.3 na 7.8 mtawalia
Post a Comment