Simba SC vs Mbao FC, mtoto hatumwi dukani FA, leo
Kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma unao wakutanisha klabu ya Simba SC dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.
Simba inahitaji ushindi katika mchezo huu baada ya kupoteza kuchukua kombe la Ligi kuu, huku ikiwa na historia ya kutoshiriki michuano ya Afrika kwa mara ya mwisho mwaka 2013, na kutolewa na Recreativo de Lobolo ya Angola kwa vipigo vya nyumbani na ugenini, ikifungwa 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na 4-0 ugenini.
Toka wakati huo klabu ya Simba imekuwa ikishuhudia jirani zake Yanga pamoja na Azam FC zikikwea pipa kwenda kushiriki michuano ya Afrika.
Kucheza mchezo huu wa leo, kwa klabu ya Simba SC ni muhimu lakini umuhimu wake zaidi ni pale klabu hii itakapo shinda taji hili na kupata fursa ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya miaka minne sasa kupita.
Klabu ya Mbao FC, ni miongoni mwa klabu ambazo zimefanya vizuri katika ligi kuu msimu huu, imeweza kumfunga Yanga katika michezo miwili timu hizi zilipokutana.
Ushindi wa 1-0 kwenye mechi ya mwisho ya Ligi Kuu dhidi ya Yanga Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kufanya timu hii kusalia katika ligi, kwa ushindi huo unaipa kiburi– Mbao FC leo itakapo kutana na mnyama, Simba SC.
Post a Comment