Header Ads

Master P na ujio wa album yake mpya

Usiite hii ni Comeback, kwa zaidi ya miaka 20 yupo katika game ya muziki  wa Hip Hop kama muasisi ana anajulikana kwa kuachia album zaidi ya 10 huyu ni Percy Robert Miller a.k.a Master P.

 Intelligent Hoodlum” ndio itakuwa album ya Master P, katika show ya Rap-Up HQ wiki hii rapa huyo aliongozana na mwanae Cymphonique, na ameeleza kuwa album hiyo itaachiwa rasmi leo Mei 27.”Album yangu ni kali nimehakikisha kuwa naweka ngoma nzuri, na bora zaidi na huu ndo muda wangu sasa” ameeleza Master P.

Intelligent Hoodlum imeshirikisha watu kama Ice Cream Man na baadhi ya kolabo yupo Silkk the Shocker moja ya memba wa No Limit family kwenye ngoma ya “I Done Seen.”Pia ngoma zingine zilizopo ni pamoja na “I Ain’t Going Back” na “Grew Up.”

No comments