Zullu atemwa Yanga
Uongozi wa Mabingwa ligi kuu Tanzania Bara Young Africans kupitia Katibu Mkuu wake Charles Boniface Mkwasa, wametangaza rasmi kuachana na kiungo mkabaji mwenye uraia wa Zambia, Justine Zullu baada ya benchi la ufundi la timu hiyo kutoridhishwa na kiwango chake.
Mkwasa amebainisha hayo mapema leo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya klabu hiyo zilizopo eneo la Kaunda, Jangwani Jijini Dar es Salaam na kusema wameachana na Zullu kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika kipindi cha nusu msimu wa kuwa na klabu hiyo ambapo hapo awali alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja.
"Tumefikia uamuzi wa kuachana na Zullu mara baada ya benchi la ufundi la kocha George Lwandamina kutoridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo kama walivyodhania hapo awali", amesema Mkwasa.
Katika hatua nyingine, Mkwasa amesema wameacha kumsajili mlinzi wa klabu ya Azam, Gadiel Michael kwa sasa hadi atakapo maliza mkataba wake na timu ya hiyo ya wanarambaramba wa vingunguti kwa kuwa dau la kuvunja kandarasi yake waliyoletewa ni kubwa wasingeweza kulipa katika kipindi hiki.
Post a Comment