TRA yataka wananchi waonefahari kulipa kodi badala ya kuchukia
.
MAMLAKA ya mapato nchini ( TRA) imewataka wananchi waonefahari kulipa kodi badala ya kuchukia na kulazimishwa kulipa.
Hayo yameelezwa leo katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi, yanapofanyika maenesho ya 24 ya wakulima(Nane nane) kitaifa, na ofisa elimu na huduma kwa walipa kodi mkoa wa Lindi, Odupoi Papaa alipozungumza na Muungwana kwenye banda la maenesho la mamlaka hiyo.
Odupoi ambae alikiri kwamba elimu kwawalipa kodi bado haijatosha, alisema ingawa kulipa kodi sio suala la hiari bali lazima kwakuwa lipokisheria, lakini kitendo cha kulipa kwa hiari ni kipimo na alama ya uzalendo.
" Wanatakiwa kuona fahari kulipa kodi kwasababu miongoni mwa uzalendo nipamoja na kulipa kodi. Hata hivyo wafanyabishara wengi wanachukia kulipa kodi ndipo tunalazimika kusukumana nao. Hata sisi hatupendi watu walipe kwa kilazimishwa, hata hivyo hatuna jinsi. Wasipolipa serikali yao wenyewe itashindwa kuwahudumia na kutekeleza miradi ya maendeleo, "alisema Odupoi.
Ofisa huyo alisema mamlaka bado inakazi na wajibu wa kutoa elimu ili wananchi ili waone fahari kulipa kodi badala ya hali ya sasa, ambapo wananchi wengi wanaiona mamlaka hiyo kama adui anaestahili kuchukiwa.
Akiwa na stika mkononi pamoja na maofisa wenzake wa idara hiyo, wakiwemo waliotoka mkoa wa Mtwara na makao makuu, Odupoi alisema :"Tunaendelea na kazi ya kutoa elimu kwenye mabanda yote, sambamba na kugawa na kubandika stika zinazohamasisha watu wadai risti baada ya kuuziwa bidhaa, tena tunahimiza utumiaji wa mashine za kielektroniki. Kwasababu bado elimu haijatosha sio kwa mkoa wa Lindi tu, bali nchini,"alisema Odupoi.
Akizungumzia zoezi la mashine za kielektroniki mkoani humu, alisema wanaendelea kuhamasisha utumiaji wa mashine hizo. Huku akibainisha kuwa baadhi ya wafanyabishara wanakwepa kutumia kutokana na hofu ya kulipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) japokuwa sio wafanyabishara wote wanasifa ya kulipa kodi hiyo. Huku akitoa wito kwa wafanyabishara watumie mashine hizo ili kuondoa utata kwenye kumbukumbu za mauzo yao. Lakini pia watakuwa wamerahisisha serikali kukusanya mapato halali na sahihi.
Odupoi pia akiwataka wananchi kudai risti kila wanaponunua bidhaa.Nakubainisha kwamba kutumia EFD sio kigezo cha kulipa kodi ya ongezeko la thamani. Bali wenye sifa hiyo ni wenye mauzo yasiyo pungua shilingi milioni miamoja kwa mwaka.
"Hata hizo mashine zinaonesha hivyo kwenye risti. Kwani mfanyabiashara asiesitahili kulipa kodi hiyo, risti inaonesha kuwa hakuna VAT,"alisisitiza.
Maenesho ya 24 ya wakulima, leo yanaingia katika siku ya tano tangu yazinduliwe tarehe 1 mwezi huu, na waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene.

Post a Comment