Rais Trump aidhinisha vikwazo dhidi ya Urusi
Rais wa Marekani Donald Trump ameusaini kuwa sheria mswada ambao utaiwekea vikwazo vipya Urusi, kwa kuingilia kati uchaguzi wa Marekani mwaka 2016.
Mswada huo ambao uliwekwa sahihi kisiri katika Ikulu ya White House pia inaziwekwa viwazo Iran na Korea Kaskazini.
Sheria hiyo inamzuia Trump kutokana na kuipunguzia vikwazo Urusi bila ya idhini ya bunge la Congress.
Urusi inakana kuingilia uchaguzi wa Marekani naye Trump akikana kushirikiana na Urusi.
Trump aliishutumu Congress ambayo wiki iliyopita ilipitisha kwa wingi mswaada huo na kuutuma kwenda Ikulu
Urusi tayari imejibu kwa kuwaamrisha wanadiplomasia 755 kuondoka kutoka ofisi zake za kibalozi.
Vikwazo hivyo vinakuja miezi kadhaa baada ta Rais Obama kuwatimua wanadiplomasia 35 wa Urusi.
Seneta wa Republican Lindsey Graham aliupongeza mswaada huo wakati ulipita.
"Rais Putin alifanya kitu ambacho hakuna yeyote nchini Marekani anaweza kukifanuya. aliileta pamoja Congress" alisena Graham.
Post a Comment