Header Ads

Rais Shein, kesho kuanza ziara ya siku 3 Mkoani Mjini Magharibi, Zanzibar

                               
                                                      Dkt Ali Mohamed Shein

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kesho anatarajiwa kuanza ziara ya siku tatu katika mkoa wa Mjini Magharibi.

Kwamujibu wa Taarifa kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini Magharibi ziara hiyo itagusia zaidi ukaguzi wa miradi ya maendeleo, uzinduzi miradi iliyokamilika sambamba na usikilizwaji wa kero za Wananchi na kuzipatia majibu.

Rais Shein anataraijiwa kuanza ziara yake kesho siku ya Ijumamosi katika wilaya ya mjini, Siku ya Ijumapili atazuru wilaya ya Mjini magharibi 'A' na siku ya Ijumatatu atamalizia katika wilaya ya Magharibi 'B'

Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Rais Shein tangu achaguliwe katika uchaguzi wa marudio mwaka jana, Na ni ya tatu tangu aingie madarakani mwaka 2010.

No comments