Header Ads

Prince Boateng ajiaunga na Frankfurt ya Ujerumani

                                                    
                                                                           Kelvin Prince Boateng

Kiungo wa kimataifa wa Ghana mwenye asili ya Ujerumani Kelvin Prince Boateng leo Ijumaa ya August 18 amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea Eintracht Frankfurt ya Ujerumani ikiwa ni siku mbili zimepita toka avunje mkataba kwa makubaliano na club ya Las Palmas ya Hispania.

Kelvin-Prince Boateng aliyejiunga na Eintracht Frankfurt leo kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kufanyiwa vipimo vya afya, alifikia makubaliano na Las Palmas ya kuvunja mkataba kwa sababu zake binafsi.

Taarifa iliyotolewa na Las Palmas kuhusiana na Boateng na alichozungumza Boateng kuwa amemua kurudi Ujerumani ili aweze kuishi na familia yake ambayo makazi yake ni Ujerumani na yeye alikuwa anafanya kazi Hispania.

No comments