Header Ads

Mbunge Heche akabwa koo



Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche amekamatwa na polisi leo alipokwenda kituo cha polisi cha Tarime alipokwenda kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake.

Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba amethibitisha kukamatwa kwa Mbunge Heche na kusema kuwa polisi wamemkamata kutokana na kauli zake ikiwepo kauli ya kutaka kilimo cha bangi kihalalishwe pamoja na kauli yake ya kuzuia shughuli za ACACIA.

"Mhe. Heche alifika Polisi Tarime leo kwa ajili ya kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake, katika hali ya kushangaza naye akawekwa chini ya ulinzi na RCO na baadae kuelezwa kuwa alikuwa.

akitafutwa kwa makosa mawili 1. Kauli aliyoitoa mapema mwaka huu katika mkutano wa hadhara Sirari ya kwamba atapeleka hoja bungeni aiombe serikali ihalalishe kilimo cha bangi na pili kauli yake ya hivi karibuni kuhusu kuzuia shughuli za ACACIA Nyamongo kufuatia Kauli ya Rais kwamba mgodi huo haupo kihalali nchini." alisema Marwa Ryoba.

Aidha Mbunge Marwa anasema kuwa Heche amekataa kutoa maelezo yoyote polisi na jeshi la polisi limechukua simu zake zote.

"Wamemwachia Heche ila wamechukua simu zake zote na kumtaka afike polisi Jumatatu kwa mahojiano. Leo amekataa kuchukuliwa maelezo yoyote kwa kuwa hakuwa amekwenda Polisi kwa mambo hayo bali kushughulikia kukamatwa kwa Katibu wake, hivyo amejidhamini na kuondoka ila simu zimebaki Polisi" alisema Marwa Ryoba.

No comments