Header Ads

Kampuni ya China yashtakiwa kwa kuchafua mazingira Gambia

                                            Ramani ya taifa la Gambia

Wanamazingira kutoka miji midogo ya pwani nchini Gambia wameipeleka kampuni moja ya China mahakamani kwa madai ya kutupa takataka za sumu kwenye bahari.

Hatua hiyo inakuja baada ya serikali kukubaliana nje ya mahakama na kampuni hiyo ya Golden Lead kumaliza tatizo hilo.

Wakazi wa eneo la Gunjur takribani kilimita arobaini kusini mwa mji Mkuu wa Banjul wamesema mamia ya samaki wamekuwa wakifa katika eneo hilo la bahari tangu kampuni hiyo ya Golden Lead ilipojenga kiwanda cha kusindika samaki katika mji huo mwaka 2016.

Wanasema watu ambao wamekuwa wakiogelea katika eneo hilo wamekuwa wakidhurika na kupata matatizo ya kiafya.

Kampuni ya Golden Lead imepinga tuhuma hizo.

Kampuni hiyo ilikubaliana kumaliza suala hilo nje ya mahakama na Mamlaka ya taifa ya Mazingira nchini Gambia mwezi uliopita.

No comments