Header Ads

HIZI NDIZO BAADHI YA DALILI ZA UGONJWA WA KANSA



Kugundua dalili za awali ni njia bora zaidi ya kutibu huu ugonjwa. Kuna baadhi ya dalili ambazo zinaonekana moja kwa moja, ingawa idadi kubwa ya wanaume na wanawake wanazipuuzia.
Hizi ni baadhi ya dalili za saratani:

1.Kupungukiwa na pumzi
Moja ya dalili ya kansa ya mapafu, ambapo wagonjwa wengi wanasema waligundua awali ni kubana kwa pumzi na kutoka kwa sauti fulani wakati wakivuta pumzi.Kwa kutogundua watu wengi wanafikiri kuwa wana asthma.

2.Kikohozi kisichoisha na maumivu ya kifua
Aina tofauti za saratani, ikiwa ni pamoja na leukemia na kansa ya mapafu, zinaweza kugundulika kwa kikohozi.
Tofauti ni kwamba hili tatizo linaweza kuwa la mda mrefu au kwa mda mfupi alafu linapotea.Kama una maumivu yasiyoisha au kikohozi kisichoisha, nenda kafanye uchunguzi.

3.Ugumu katika kumeza
Kupata ugumu kumeza ni moja ya dalili inayohusiana na kansa ya kizazi au ni dalili za awali za kansa ya mapafu.

4.Kupungua uzito
Kama ukigundua uzito wako umepungua bila ya kufanya diet au kubadilisha mfumo wako wa maisha,yakupasa kujiuliza kwanini.Kupungua uzito ni moja ya dalili ya colon cancer, ambayo inaathiri hamu ya kula na mwili kushindwa kutoa uchafu vizuri.

5.Kucha kubadilika rangi
Kubadilika kwa kucha ni moja ya dalili za aina tofauti za saratani. Mistari ya Brown au weusi au vidoa kwenye kucha, ni alama ya kansa.Kucha rangi ya Pale au nyeupe ni alama kwamba ini lako alifanyi kazi vizuri, na ni moja ya dalili ya saratani ya ini.

Ukiona mabadiliko yeyote yasiyo kawaida katika mwili wako,ni vyema ukaenda katika vituo vya afya ukafanyiwe uchunguzi.

No comments