Grace Mugabe anusurika
Baada ya kupewa kinga ya kidiplomasia na serikali ya Afrika Kusini, mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe amerejea nyumbani siku ya Jumapili, licha ya miito kwamba ashitakiwe kwa madai ya kumshabulia mwanamitindo mmoja mjini Johannesburg.
Shirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC lilimuonyesha Grace Mugabe akisalimiana na maafisa wa serikali na jeshi katika uwanja wa ndege wa Harare baada ya kushuka kwenye ndege ya shirika la ndege la Zimbabwe pamoja na mume wake, ambaye alihudhuria mkutano wa kilele wa viongozi wa kanda ya kusini mwa Afrika mjini Pretoria.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane, ilimpa kinga ya kidiplomasia Grace Mugabe kupitia taarifa iliyochapishwa katika gazeti la serikali siku ya Jumapili.
Awali polisi ya Afrika Kusini ilitoa tahadhari ya kiusalama kwenye maeneo ya mipakani kuhakikisha anakamatwa
na vyombo vya sheria ambapo baadaye ulitolewa uamuzi wa serikali kuhusu maombi ya kinga kwa mke wa Rais.
Mwamitindo Gabriella Engels alimshtumu Bi Mugabe kwa kumpiga na kumjeruhi baada ya kumkuta akiwa na vijana wake wawili wakiume katika hoteli huko Sandton mjini Johannesburg.
Post a Comment