Header Ads

Anachokisema Diamond kuhusu Chibu Beats


Baada ya ukimya wa muda mrefu tangu msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz atangaze ujio wa bidhaa zake za headphone ‘Chibu Beats’, msanii huyo ameelezea kinachochelewesha.

Muimbaji huyo ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa bidhaa hizo zimechelewa kutokana na mchakato wa usajili wa jina.

“Katika usajili wa Chibu Beats jina lilileta matatizo kidogo, ilikwamisha hapo kwa sababu neno beats mtu kashalisajili dunia nzima mtu mwingine asilitumie neno la beats, siunajua ni la Dre. Kwa hiyo tunaweka namna nyingine ambayo itakuwa nzuri, zitatoka zimeshakuwa tayari mpaka sampo, tumeshasikiliza ni fresh sound hatari” amesema Diamond.

No comments