Header Ads

Mwanafunzi chuo Kikuu ajinyonga




Mwanafunzi huyo Fredrick Kinyanjui, 22,wa Chuo Kikuu huko Shauri Moyo, Jijini Nairobi amejiua baada ya kupita wiki mbili tangu arudishwe nyumbani kwa kukosa ada.

Mwanafunzi huyo alikuwa mwaka wa pili katika Chuo cha Multimedia, alikutwa akiwa amejinyonga kwenye paa la nyumba yao jana jioni.

Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Buruburu DCI, Jeremiah Ikiao alisema kuwa, wachunguzi wamebaini mwanafunzi huyo alirudishwa nyumbani siku 14 zilizopita kwa kukosa ada.

DCI Ikiao amesema mama wa Kinyanjui alikuwa ameenda kazini wakati mwanafunzi huyo alipochukua uamuzi wa kujinyonga.

No comments