Messi apendekeza usajili,,,,,,,,
Hispania. Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ameshauri Riyad Mahrez wa Leicester City, Marco Verratti kutoka PSG na Philippe Coutinho wa Liverpool wawekwe kwenye mipango ya usajili klabuni hapo.
Miamba hiyo ya Hispania imemaliza nafasi ya pili msimu huu kwenye La Liga baada ya Real Madrid kunyakua taji la ubingwa.
Hata hivyo, zigo la usajili limemwangukia kocha mpya, Ernesto Valverde alipewa mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo akitokea Athletic Bilbao.
Mchezaji Messi anaushawishi mkubwa kwenye klabu hiyo, na hiyo siyo mara ya kwanza kutoa ushauri wa kusajiliwa wachezaji muhimu na jambo hilo lilitekelezwa.
Mahrez ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Leicester City kutwaa taji la Ligi Kuu England msimu wa 2015/16 na kuiwezesha kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ulioisha.
Post a Comment