Marekani yaionya China kuhusu visiwa bandia baharini
Marekanai hautakubali China kuweka wanajeshi kwenye visiwa ilivyojenga Kusini mwa bahari ya China, waziri wa ulinzi wa Merekani James Mattis ameonya.
Akiongea katika mkutano wa kiusalama huko Singapore, Bwana Mattis amesema kwamba hatua ya Uchina ya kutengeneza visiwa bandia na kuongeza uwepo wake wa kijeshi katika bahari ya kimataifa unahatarisha amani katika eneo hilo
Hata hivyo amesema ugomvi kati ya Marekani na Uchina unaweza kuepukika, na akaipongeza Uchina kwa juhudi zake za kukabiliana na mgogoro unaotokana na uundaji wa zana za kinyuklia nhini Korea Kaskazini.
Matamshi hayo yanatolewa muda mfupi baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kufuatia majaribio kadha ya makombora mwaka huu
Baraza hilo liliunga mkono kwa wingi vikwazo hivyo baada ya mazungumzo ya majuma kadha kati ya Marekani na China.
Post a Comment