Makabiliano ya silaha bungeni Iran
Kundi linalojiita Dola la Kiislamu limedai kuhusika na mashambulizi mawili yaliyoteka kwa mfululizo leo hii mjini Tehran, Iran ambayo yanatajwa kusababisha vifo vya hadi watu saba na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Kundi linajiita Dola la Kiislamu limedai kuhusika na mashambulizi mawili yaliyoteka kwa mfululizo leo hii mjini Tehran, Iran ambayo yanatajwa kusababisha vifo vya hadi watu saba na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Washambuliaji kadhaa wamelishambulia bunge la Iran na mtu alijitoa muhanga alilenga eneo la kaburi la mwanzilishi wa mapinduzi ya Iran hayati Ayatollah Ruhollah Khomeini na kusababisha kifo cha mlinzi na kujeruhi watu wengine 12 katika kile kinachotajwa kuwa mashambulizi ya nadra kutokea. Hayo yanafanyika wakati mizizimo ya risasi ikiendelea katika jengo la bunge.
Kundi la linalojiita dola la Kiislamu IS limedai kuhusika na mashambulizi hayo kupitia mtandao wake wa habari wa AMAQ. Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran IRNA-tukio hilo lisilo la kawaida lililotokea katika mji mkuu wa Iran, Tehran, limesababisha Wizara ya Ulinzi kuitisha mkutano wa usalama wa dharura. Vyombo vya habari nchini humo vinasema helikopta za polisi zinazunguka jengo la bunge na kwamba mawasiliano ya simu zote za mkononi kwa walio ndani ya jengo hilo yamekatwa.
Sakata katika eneo la bunge
Nalo shirika la habari la ISNA linasema milango yote ya kuingilia na kutoka imefungwa na wabunge na waandishi wa habari ambao walikuwemo katika jengo hilo wakati vikao vikiendelea wameamriwa kutulia katika eneo maalumu. Lakini Televisheni ya serikali baadae ilisema waashambuliaji wanne wanahusika katika shambulizi la bungeni, na kwamba watu wanane wamejeruhiwa. Televisheni hiyo ilimnukuu mbunge mmoja Elias Hazrati aliyesema washambuliaji hao walikuwa wamejihami kwa bunduki aina ya Kalashnov.
Vilevile televisheni hiyo ilisema mlinzi aliuwawa na watu wengine wanne wamejeruhiwa katika shambulizi hilo la kwenye eneo la kaburi la Khomeini. Mmoja ya washambuliaji aliuliwa na mlinzi na kuna mwanamke aliyetiwa mbaroni. Chombo hicho kiliwaelezea washambuliaji katika eneo la kaburi kama "magaidi" na kuongeza kuwa mmoja alifanya shambulizi la kujitoa muhanga pasipo kutoa ufafanuzi zaidi.
Pamoja na shambulizi katika eneo la kaburi la Khomeini hatari lakini kaburi la kiongozi huyo limekuwa alama muhimu kwa taifa hilo. Kama kiongozi wa kwanza wa Iran, Khomeini alikuwa kuongozi muhimu wa taiifa hilo na alikuwa kiongozi wa kimapinduzi ya mwaka 1979.
Afisa mwanadamizi ambaye hakutaka kutaja jina lake ameilezea hali kuwa mbaya na kuyataja mashambulizi hayo kuwa pigo kwa rais wa nchi hiyo Hassan Rouhani, akihoji inakuwaje bunge lenye ulinzi mkali likashambuliwa.
Rouhani alisalia madarakani baada ya ushindi wa kishindo dhidi ya mgombea mwenye msimamo mkali wa kihafidhina na vikosi vya ulinzi wa Jamhuri, ambavyo ndiyo vyenye nguvu zaidi nchini Iran. Televisheni ya Iran imesema bunge limerejea shughuli zake na kuonyesha picha za kile ilichosema ni kikao cha ufunguzi kikiendelea kama kawaida.
Post a Comment