MAJIBU YA SHETTA KWA ALI KIBA NA DIAMOND
Mwimbaji staa wa Bongofleva Shetta leo June 2, 2017 kupitia Leo Tena ya Clouds FM amesema kuwa hana team yoyote kati ya zinazotajwa kuwa team za mashabiki kwa baadhi ya wanamuziki wa Bongofleva badala yake yeye ni Team Shetta.
Kauli ya Shetta imekuja baada ya kuulizwa swali la moja kwa moja na mmoja wa mashabiki wake kupitia kipindi hicho ambaye alitaka kujua yuko upande upi kati ya zinazotajwa kuwa team za mastaa Alikiba na Diamond platnumz.
Shetta amesema hana team na haamini kama kuna team baina yao lakini amedai kuwa anawakubali wote kwa kuwa ni wasanii wenzake na marafiki zake pia:>>>“Mimi sina team bro, mimi ni team Shetta hao wote ni washikaji zangu, wasanii wenzangu na ndugu zangu…kwanza kuna ma-team? Sijui kama kuna team ila mimi team Shetta” – Shetta.
Mbali na hayo, Shetta ametoa ahadi kwa mashabiki wake akisema atawaletea wimbo mpya hivi karibuni ambao tayari video yake ameifanyia Dubai ambako alikuwa na show akiahidi kuutoa mwisho wa Mfungo wa Ramadhani video na Audio.
Post a Comment