Ruvu Shooting Yaendelea Kujifua Tayari Kwa Ligi Kuu Ya Vodacom Tanzania Bara

RUVU SHOOTING
TIMU ya soka ya Ruvu Shooting yenye mskani yake Ruvu Mlandizi, Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani wanaendelea na mazoezi makali ikijiwinda na michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara masimu wa 2017/2018 inayotaraji kuanza mwezi wa nane.
Mwandishi wa habari hizi alitembelea kwenye kikosi cha timu hiyo na kuwashuhudia wachezaji wakijifua vilivyo chini ya kocha Suleiman Mtungwe, Exvian Owen na kocha wa makipa Godhard Misweku huku wachezaji wakionesha kujituma vilivyo kwenye mazoezi hayo yaliyochukua zaidi ya masaa mawili.
Wachezaji hao waliofika uwanjani saa 9.30 jioni wakifanya mazoezi ya kukimbia kuzunguka uwanja, ya viungo kabla ya kucheza mpira kukiwa na timu tatu hali iliyolazimu moja kusubiri itayofungwa lakini hata hivyo mchezo wa awali hakuna iliyopata ushindi pamoja na timu moja kupata penati liyopigwa na Kisuke Kisuka iliyoota mbawa huku kipa Bidii Hussein akiwa ameshapotea langoni.
Timu ya pili iliyoingia ikiongozwa na mchezaji mkongwe Mangasin Mbonos ilipambana vikali na wachezaji wa timu inayoundwa na wachezaji walioshiriki Ligi msimu uliomalizika wakiwemo chipukizi waliweza kupata ushindi wa bao 1-0 lililoonekana kumchanganya kipa namba moja wa kikosi hicho Abdallah Abdallah.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mazoezi hayo mbali ya makipa Bidii na Abbdallah wengine ni Said Madega, Shaibu Nayopa, Kassimu Daby, Fullu Maganga, Yussuph Nguya, Shaaban Nsalla, Ayoub Kitala, Mbonosi, Kisuke, Mohamed Njaid, Hamis Kasanda, Abdul Mpamnila na wengine kadhaa.
Katika mazoezi hayo yenye ushindani mkubwa yaliyochukua zaidi ya dakika 120 inaonekana wazi kwamba jopo la makocha wa timu hiyo watalazimika kuwa na kazi ya ziada katika kutengeneza kikosi kitachopeperusha vema bendera yao kwenye kinyang'anyiro cha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2006/2007 unaotaraji kuanzamwezi ujao.
Shooting iliyoanza kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2005/2006, mara zote imefanya vizuri tangu kipindi hicho ambapo pamoja na kwamba kuna mwaka inashuka lakini inarudi tena katika msimu unaofuata hali inayothibitisha kuwa na wachezaji wenye uwezo sanjali na uongozi wake.
Ligi hiyo inayotaraji kuanza kutimua vumbi kuanzia mwezi wa nane, Ruvu Shooting itaanza kutupa kete yake ya kwanza kwa kupambana na Simba kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo unaotazamiwa kuwa wa ushindani kutokana na maandalizi ya timu hizo.




Post a Comment