Header Ads

Real Madrid Mabingwa wa Champions League 2016/17




Usiku wa June 3 2017 jijini Cardiff nchini Wales ilikuwa ni siku ya kihistoria katika uwanja wa Millenium mahali ambapo anatokea staa wa Real Madrid Gareth Bale, usiku huo Real Madrid walicheza game yao ya fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Juventus.



Real Madrid ambao ndio walikuwa Mabingwa watetezi wa taji hilo wamefanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga Juventus magoli 4-1, Cristiano Ronaldo ambaye ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga jumla ya magoli 12 alifunga magoli dakika ya 20 na 64.



Casmiro ndio alikuwa staa wa Real Madrid aliyefunga goli la pili dakika ya 61 na Asensio akafunga goli la nne dakika ya 90, Juventus walifanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya 27 kupitia kwa Mandzukic na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko magoli yakiwa 1-1.



Ushindi huo sasa unaiwekea Real Madrid kuendelea kuwa club iliyotwaa mataji mengi ya Champions League kwa kutwaa taji la 12, AC Milan wao wanaendelea kuwa nafasi ya pili kwa kutwaa taji hilo mara 5, Ronaldo anaendelea kuweka rekodi ya kumfunga Buffon goli 7 wakikutana kwa mara ya 5 wakati mpinzani wake Messi ameshindwa kumfunga Buffon hata mara moja.



Kufunga magoli mawili kwa Ronaldo kumemfanya kufikisha jumla ya magoli 600 katika maisha yake ya soka akifunga kwa ngazi ya club na timu ya taifa, Ronaldo pia anaendela kuwa mchezaji pekee aliyewahi kufunga magoli kuanzia 10 katika michuano ya Champions League katika misimu sita mfululizo, Real watacheza na Man United August 8 UEFA Super Cup.

No comments